STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa
siku alipokuwa mahakamani akisomewa kesi inayomkabili ya kumuua bila
kukusudia msanii mwenzake, marehemu Steven Kanumba, alipata mchecheto
sana.
Akipiga stori na paparazi wetu alisema, siku hiyo wakati kesi
ikiendelea, alipata mchecheto kiaina na kujikuta ghafla akiwaza juu ya
hatima yake hivyo kuangukia katika lindi la hofu.
“Daah! Nilipata mchecheto ghafla hata sijui kwa nini, nilivuta picha
ya mbali sana na kujikuta nikijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na
majibu,” alisema.
Msanii huyo alisomewa shitaka lake hilo Februari 17, mwaka huu kwenye
Mahakama Kuu, jijini Dar, kesi hiyo iliahirishwa hadi itakapotajwa tena
baada ya msanii huyo kujibu maswali ya kweli au si kweli.
No comments:
Post a Comment