Pages

Thursday, March 6, 2014

POZI LA MASOGANGE, MWANAUME UTATA!

PICHA mpya ya ‘video queen’ matata Bongo, Agnes Jerald ‘Masogange’ na mwanaume mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja, imezua utata kutokana na ukaribu wao.
Agnes Jerald ‘Masogange’ katika pozi na mwanaume ambaye hakujulikana jina lake.
Picha hiyo ilitupiwa katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita huku ikisindikizwa na maneno kuwa wawili hao ni wapendanao hali iliyosababisha wadau wengi kupongeza kuwa ni kapo nzuri.
“Mh! Kapo nzuri jamani, atulie sasa hapa Masogange,” mmoja wa wachangiaji alipongeza. Alipotafutwa Masogange kwa njia ya simu, hakupokea! Jitihada zinaendelea kuondoa utata huo.

No comments:

Post a Comment