Pages

Wednesday, March 5, 2014

Ray C amtaka Lord Eyez kubadilika

 
Staa nguli wa muziki wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila’Ray C’amemtaka aliyekuwa mpenzi wake, Lord Eyez kubadilika kutokana na changamoto za maisha zinazomkuta hasa ya kutuhumiwa mara kwa mara kuiba mali za watu. 
Msanii huyo wa hip hop kutoka kundi la Weusi,Lord Eyez anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa kuvunja gari na kuiba laptop huko Arusha,ambapo Kundi lake la Weusi limetoa tamko kuhusu msanii huyo kutoka na natukio hilo.Kupitia account yake ya Instagram aliandika hivi…Badilika babaa......Nakuombea sana ujitambue na ubadili mwendo wa Maisha yako...Wewe bado ni kijana mdogo sana na una kipaji cha pekee.....Kila Mtu Ana changamoto yake ya maisha,angalia wapi ulipokosea,litambue tatizo halafu kubali kwamba una tatizo then rekebisha Hilo tatizo.


Anza Maisha mapya,Badilika.........Majanga yote yanayokukuta ni ishara tosha kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba unakoelekea siko,Kama una akili timamu basi utagundua Hilo na utajirekebisha babaa,Nakuombea kila la kheri katika mabadiliko ya Maisha yako...........Karibu Kwenye Tiba ya Methadone...................Methadone Kiboko ya Madawa.
Kwa mujibu wa Ray C aliwahi kusema kuwa Lord Eyez ndiye mpenzi wake alimuingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya lakini sasa ameshaacha na kuanzisha taasis yake ya Ray C Faundation ya kupiga vita utumiaji wa madawa hayo.

No comments:

Post a Comment