Vyombo vya habari vya Uingereza, likiwemo Mail on Sunday vimeripoti
kuwa David Moyes ataachishwa kazi wiki chache zijazo na kwamba anaweza
kuachiswa hata leo au kesho.
Wamiliki wa timu hiyo, familia ya Glazer wanadaiwa kuishiwa uvumilivu
kwa kocha huyo ambaye tangu aanze kuinoa imeendelea kufanya vibaya na
sasa ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Barclays Premier League.
Siku ya jumapili Man United ilifungwa mabao 2-0 na Everton.
Uongozi wa juu wa klabu ulikuwa umepania kumpa muda kocha huyo lakini
umeona ni ngumu kuona mabadiliko kwakuwa hata wachezaji hawamwamini
tena kocha wao. Ripoti hizo zinadai kuwa nafasi yake inaweza
ikachukuliwa kwa muda na Ryan Giggs huku makocha wanaowaniwa kuchukua
nafasi ya muda wote wakitajwa kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp, kocha wa
Uholanzi, Louis van Gaal na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.
No comments:
Post a Comment