Inatia moyo na kufurahisha mno wamama wanapoweza kufanya jambo kubwa kama hili walilolifanya wamama wa Mito ya Baraka Kariakoo! Leo kwa pamoja waliamua kutembelea kambi ya wazee na wakoma Nungwi Kigamboni na kutoa zawadi nyingi yakiwemo mabati, mbao, misumari, nyavu za madirisha, king'amuzi, nguo, simu, saa na vitu mbali mbali.
Wanawake hao walioongozwa na mwenyekiti wa wamama Mch Caroline Peter Kilango walipofika kambini hapo walianza kwa kutoa neno la uzima kwa wenyeji na baadae zawadi jambo lililowafurahisha sana wazee na wakoma hao.
Wamama hao hawaishii hapo kesho ni zamu ya kutembelea baadhi ya hospitali na kutoa misaada!
IRENE MWAMFUPE JAMII BLOG INAWAPONGEZA SANA WAMAMA WA MITO YA BARAKA KWA UPENDO WALIOOUONYESHA KWA KIPINDI HIKI CHA PASAKA MUNGU AWABARIKI SANA.
Pages
▼
No comments:
Post a Comment