Pages

Friday, April 25, 2014

WEMA AWASHUKURU WASOMAJI, GLOBAL PUBLISHERS

Mhariri wa gazeti la Ijumaa, Amran Kaima (kushoto) akimkabidhi Wema kitita chake. Anaeshuhudia ni mratibu wa matukio Global, Luquman Maloto.
Kile kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa gazeti hili kilichopewa jina la Ijumaa Sexiest Girl 2013/14, kimefikia tamati ambapo mwanadafada Wema Isaac Sepetu, amewafunika mbaya washiriki wengine na kunyakua taji hilo sambamba na kitita cha shilingi milioni moja.
Wema alitangazwa mshindi mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem na kuwafunika wenzake, Jokate Mwegelo, Jacqueline Wolper, Elizaberth Michael ‘Lulu’ na Nelly Kamwelu. Akikabidhiwa mshiko wake huo, Wema aliishukuru Global Publishers kwa kuandaa shindano hilo pia wasomaji kwa kumfanya aibuke mshindi.
“Sina la kusema zaidi ya kuwashukuru sana Global pamoja na wasomaji wa Gazeti la Ijumaa,” alisema Wema.

No comments:

Post a Comment