Pages

Wednesday, May 28, 2014

WAMBURA KUKATA RUFAA KUPINGA KUSIMAMISHWA

WAMBURA

Mgombea wa urais katika klabu ya Simba aliyeondolewa kugombea na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo, atakata rufaa.
Michael Richard Wambura ameondolewa kushiriki uchaguzi kwa kuwa si mwanachama.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, Wambura alisimamishwa uanachama kutokana na kitendo chake cha kuipeleka Simba mahakamani, lakini hakuwahi kurudishwa.

Lakini Meneja wa kampeni wa Wambura, Majaliwa Mbasa amesema watakata rufaa.

“Tutakata rufaa TFF kupitia kamati ya rufaa na tunaamini Wambura atapata haki yake agombee.
“Sisi tunaona si sawasawa kabisa, hivyo hatuwezi kuacha hili suala lipite tu,” alisema Mbasa.

No comments:

Post a Comment