UONGOZI wa Yanga umesema haujamuacha kiungo mkabaji, Athumani Idd ‘Chuji’.
Hiyo ni siku chache tangu kuwepo kwa taarifa za kiungo huyo kuachwa.
Akizungumza
na Championi Jumatatu, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema Chuji
bado ni mchezaji wao mwenye mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Njovu
alisema hadi hivi sasa, hakuna mchezaji yeyote watakayemuacha kwa wale
wote wenye mikataba mirefu ya kuendelea kuichezea Yanga.
“Hizo zote
zinazozungumzwa ni tetesi na siyo habari rasmi kutoka kwa viongozi,
Yanga haina mpango wa kumuacha mchezaji yeyote mwenye mkataba na Yanga.
“Yanga
hivi sasa ipo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwa ajili ya
kuwasajili kwenye msimu ujao, ninaamini yakiendelea vizuri haraka
tutawasajili,” alisema Njovu.
No comments:
Post a Comment