WASANII wawili wa filamu, Nice Mohamed ‘Mtunisi’ na
Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ ambao walikuwa wapenzi kabla ya kuachana na
mwanaume huyo kuoa, sasa wamerudiana rasmi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho jirani na wasanii hao kimesema
wawili hao hivi sasa wanapika na kupakua.Kilisema baada ya kurudiana,
kwa sasa wanaishi pamoja kama mume na mke maeneo ya Sinza, jijini Dar es
Salaam huku wakiishi kwa amani na upendo.
“Yaani sasa hivi Batuli na Mtunisi wana mahaba niue kwani wanaishi
pamoja wanaamka na kulala wote maeneo ya Sinza-Mawela lakini wanafanya
kuwa ni siri yao, hawataki watu wajue,”kilisema chanzo hicho.
Hivi
karibuni Batuli aliweka picha ya Mtunisi katika akaunti yake kwenye
mtandao wa Instagram na kuandika maneno haya “Alichokipanga Mungu hakuna
wa kukipangua.”
Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Batuli alisema hawezi kuzungumzia
katika vyombo vya habari kwa vile mambo hayo ni maisha yake binafsi.
Kwa upande wake, Mtunisi alicheka na kudai kusikia kutoka kwa watu
juu ya mwenzake kuweka picha yake mtandaoni na kuandika maneno ya
kimahaba, kitu alichosema hawezi kuzuia nafsi ya mtu kumuweka moyoni.
CHANZO NI GPL
No comments:
Post a Comment