Pages

Saturday, June 21, 2014

MASHABIKI WALILIA PENZI LA RAY, JOHARI

MASHABIKI wa sinema za Kibongo wamefunguka kuwa wanapenda uhusiano waliouita wa kimapenzi kati ya Wakurugenzi wa RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Blandina Chagula ‘Johari’.

Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’
Ishu hiyo ilijidhihirisha wazi juzikati mjini Dodoma wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wamekwenda kuzindua video ya wimbo wa Tuulinde Utanzania katika Uwanja wa Jamhuri.
Mashabiki walidai wanapenda kuwaona wawili hao wakiwa pamoja ingawa wenyewe wamekuwa wakikanusha kuwa hawakuwahi kuwa wapenzi zaidi ya kazi.
Mkongwe wa tasnia ya filamu Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’.
“Tunapenda kuona Johari na Ray wapenzi maana ni watoto wa mji wa Dodoma na tunawakubali sana,” alisema shabiki mmoja aliyetambulisha kwa jina la Ally.
CHANZO NI GPL

No comments:

Post a Comment