Pages

Wednesday, June 4, 2014

NIGERIA YAKOMAA NA UGIRIKI 0-0

UGIRIKI na Nigeria wametoka safe ya bila kufungana katika mechi yao ya kujiandaa kwa Kombe la Dunia usiku wa jana Uwanja wa Philadelphia Union.
Kulikuwa kuna nafasi chache za kufunga zilizotengenezwa katika mchezo huo wa mwisho mwisho wa maandalizi kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia Juni 12. 
Super Eagles: Nigeria imetoa sare na Ugiriki jana 
Nafasi nzuri zaidi waliipata Ugiriki dakika ya 83 wakati shut la Giorgios Samaras lilipozuiliwa kutoka umbali wa mita 10 na Dimitris Salpingidis akafuatia kupiga kichwa lakini akakosa pia.
Nigeria ambayo ipo Kundi F pamoja na Iran, Argentina naBosnia- ilipata nafasi nzuri nayo dakika ya 87 wakati Ogenyi Onazi alipofumua shut kutoka umbali wa mita 25 ambako liliokolewa na kipa Stefanos Kapino.

No comments:

Post a Comment