Baba yetu mpendwa Mzee Obel Benson Mwamfupe. Leo umetimiza mika tisa tangu siku Mwenyezi Mungu alipokuita kwenye makao yake. Tunakukumbuka sana kwa busara, nasaha na upendo wako kwetu. Hatujaweza kamwe kuliziba pengo ulilotuachia, lakini hekima yako na upendo uliotupa vimekuwa ni taa ya maisha yetu.
Unakumbukwa na mke wako, dada, wadogo zako, watoto, wakwe, wajukuu, vitukuu pamoja na ndugu na marafiki zako.
Ee Mwenyezi Mungu umjalie baba yetu raha ya milele. Amina
No comments:
Post a Comment