Pages

Saturday, June 28, 2014

WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA MWANANYAMALA WAKABIDHIWA VIFAA

Wauguzi wa Hospitali ya Mwananyamala wakifurahi baada ya kukabidhiwa vifaa maalumu kwa ajili ya huduma ya uzalishaji.
Baadhi ya manesi wakiwa na mwakilishi wa Upendo Women's Group Belgium baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya kupunguza matatizo ya kina mama wajawazito katika Hospitali ya Mwananyamala.

Bi Begum Chunny, ambaye ni mwakilishi wa watanzania waishio Ubeligiji akitembezwa katika wodi ya mama wajawazito.
Mama huyu  mjamzito alikuwa anasubiri ndugu zake waje ili anunuliwe vifaa vya kujifungulia ila Bi Begum alijitolea fedha kiasi.
Mganga Mkuu Hospital ya Mwananyamala Bw.Ngonyani akiwa katika pozi.
Mwakilishi wa Upendo Women's Group Belgium Bi Begum akimsalimia mama mjamzito katika wodi ya wazazi, kushoto ni Muuguzi SP Mashauri IPDM Impatient Department Manager.
Stendi maalumu kwa ajili ya drip nazo zilitolewa na Upendo Women's Group Belgium.
Wauguzi wakikabidhiwa kitanda maalumu.
Mpira huu maalumu kwa ajili ya kutandikwa eneo mama mjamzito analojifungulia.
Moja ya wodi ya kina mama wajawazito katika Hospital ya Mwananyamala.
BAADHI ya watanzania wanawake wanaoishi nchini Ubeligiji kupitia Upendo Women’s Group Belgium wamekabidhi baadhi ya vifaa katika wodi ya wajawazito hospitali ya Mwananyamala kwa kumtuma mwakilishi  wao ambaye yuko hapa nchini.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi 2,493,000/= ni pamoja na Litman Stethoscope, Ambu bag Paedreatic Bp Machine, drip stand, suction, emergency stretcher na vinginevyo.
Na Gabriel Ng’osha /GPL

No comments:

Post a Comment