Pages

Tuesday, July 1, 2014

MAXIMO, LEONARDO WAONGOZA MAZOEZI YANGA

Kocha wa Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo akisimamia leo Coco Beach.
Wachezaji wa Yanga wakipasha.
Kiungo mpya wa Yanga, Mbrazil, Coutinho (7) akipasha na wenzake.

Kiungo Coutinho na wenzake wakiendelea na mazoezi leo.
Kocha Maximo akimuelekeza jambo mshambuliaji Jerry Tegete.
Coutinho (juu) akifanya mazoezi na beki Yusuf Ngao.
Kocha mpya wa Yanga,  Mbrazili, Marcio Maximo leo Jumanne ameanza rasmi kuifundisha timu hiyo kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar.
Maximo  aliongozana na msaidizi wake Mbrazili, Leonardo Neiva  ambapo kwa pamoja waliwapa mazoezi ya nguvu wachezaji wa Yanga sambamba na kuwapa mbinu mbalimbali ili kuhakikisha anarejesha pumzi kwa vijana wake wanaojiandaa na Ligi Kuu Bara ionayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24  mwaka huu pamoja na michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
(PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL) 

No comments:

Post a Comment