MALKIA wa muziki wa Taarab Afrika Mashariki, Khadija
Omary Kopa amewachana mastaa wa kike wasioheshimu waume zao kwa
usupastaa wao, akisema suala hilo limewafanya washindwe kudumu katika
ndoa zao.
Malkia huyo alitoa dongo hilo juzikati wakati alipokuwa akipagawisha
mashabiki wake katika ukumbi wa Meeda uliopo Sinza Mori jijini Dar
alipokuwa jukwaa moja na bendi ya Extra Bongo, akiimba nyimbo zake mbili
za Fahari ya Mwanamke na Full Stop.
“Mwanamke unajiona staa mbele ya mumeo kisa supastaa, eti inafikia
hatua hadi unaachika! mwanamke unapaswa uwe na heshima kwa
mumeoeeee!”alisema mkali huyo na kuitikiwa kwa shangwe na mashabiki wake
kibao waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.
No comments:
Post a Comment