Pages

Wednesday, August 6, 2014

SHILOLE: YEMI ATAFIA UGENINI


IKIWA imesalia siku moja kuelekea Tamasha la Usiku wa Matumaini, Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa, diva kunako muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametupa kijembe kwa staa wa Nigeria aliyekuja kukinukisha Bongo, Yemi Alade kuwa amekuja kufia ugenini.Diva kunako muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.

Akizungumza na Risasi Vibes, Shilole anayetamba na ngoma ya Namchukua, alijibu tambo za Yemi ambaye alimtambia kuwa amekuja Bongo kumteketeza.
“Yemi amekuja kukutana na balaa la mwaka.Siwezi kukubali kuiaibisha nchi yangu kwa kufunikwa na yeye. Lazima nimuoneshe jeuri anitambue mimi ni nani. Jeshi langu limeshajipanga na niseme tu kuwa kaja kuteketezwa Bongo,” alisema Shilole.Yemi Alade.
Tamasha la Usiku wa Matumaini linatarajiwa kufanyika keshokutwa huku burudani kibao zikitegemewa kutawala uwanjani hapo kama vile, ndondi, muziki wa Injili, soka na mengine kibao.

No comments:

Post a Comment