Pages

Tuesday, September 2, 2014

EXCLUSIVE: YANGA YAIVUTA CRDB, KUINGIA MKATABA LEO, YAIACHA BENKI YA POSTA




Kuna taarifa kuwa Yanga imemalizana na Benki ya CRDB na huenda leo wakaingia mkataba wa awali.
Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa Yanga imeamua kuachana na Benki ya Posta (TPB) ambayo iliingia nayo mkataba sambamba na klabu ya Simba pia.
Lakini Yanga imeamua kujiengua na kutafuta wadhamini wapya huku ikifanikiwa kuwapata CRDB.
“Kweli Yanga wanaingia mkataba na CRDB na tumeambiwa kuwa wameishafanya utaratibu wa kuvunja mkataba na TPB,” kilieleza chanzo.
Viongozi wote wa Yanga, hawakutaka kulizungumzia suala hilo huku wakisisitiza utafanyika mkutano wa waandishi leo na mambo yote yatawekwa hadharani.

No comments:

Post a Comment