Pages

Saturday, September 27, 2014

MZIKI MNENE WA EFM WATIKISA BAGAMOYO

Mashabiki wa  kituo kipya cha EFM 93.7 Radio wakicheza Mziki mnene ndani ya Bagamoyo.
Mashabiki wakiendelea kupagawa na burudani.
Mashabiki waliojitokeza Bagamoyo hii ni ishara kwamba Efm inasikilizwa sana.
EFM 93.7 Radio  kituo kipya kabisa jijini Dar es salaaa bado kinaendelea kujiimarisha huku kikijizolea maelfu kwa  maelfu ya mashabiki. Kwa sasa Efm Radio inaendesha Kampaini ya Mziki menene Bar kwa Bar.
Lengo la Kampaini ni kuwakutanisha watanzania sehemu mmoja na kuwashukuru kwa mapokezi mazuri waliyoipa Radio hiyo tangu kufunguliwa kwake hadi sasa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Vipindi wa EFM Dickson Ponela hii ni ishara kwamba Efm inasikilizwa sana na watu wameikuli na wanaendelea kuikubali.
Dickson Ponela ameongeza kuwa kampeni hii ya Mziki Mnene itaendelea kwa takribani wiki 12 na itazunguka maeneo ya Kibaha,Ukonga,Kigamboni,Ilala,Kinondoni,na Temeke.

Amefafanua kuwa wasikilizaji wao wamewashika mkono na kuwaonyesha njia nzuri ya kupita sasa na sisi ni wakati wetu wakuwaburudisha hakuna kiingilio.
Mziki Mnene inawakutanisha Madj wakali kutoka Efm Radio kama Dj Skit, Dj Timba na Dj X5.

No comments:

Post a Comment