AKANUSHA! Baada ya tetesi kuzagaa kuwa aliyekuwa
Miss Progress International, Julieth William kuwa ana mtoto mchanga,
mwenyewe ameibuka na kufunguka kwamba habari hizo ni za kizushi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Julieth alisema anashangazwa na
maneno hayo ya watu kwamba ana mtoto wakati hajawahi kuzaa hivyo
anaumizwa sana na tetesi hizo.
“Sijawahi kuzaa jamani nawashangaa wanaoeneza habari kwamba nina
mtoto, mara nyingi nakuwa na watoto wa ndugu zangu hata hivi karibuni
nilikuwa na mtoto mchanga maeneo ya Mlimani City, naumizwa sana na
habari hizi za uongo,”alisema Julieth.
No comments:
Post a Comment