Pages

Thursday, October 2, 2014

MAZITO YAIBUKA MUME WA BAHATI BUKUKU KUOA TENA

Na Shani Ramadhani
IMEVUJA! Mwimba Injili mwenye kasi ya juu, Madam Ruth anadaiwa kuwa ndiye mshenga katika lile sakata la mume wa staa wa nyimbo hizo Bongo ambaye wametengana, Bahati Bukuku, Daniel Basila kutaka kufunga  ndoa na mwimba Injili mwingine, Elizabeth Ngaiza ‘Lizy’.
Kwa mujibu wa chanzo cha ndani, Madam Ruth ambaye anatamba na albamu za Jana Imepita na Kesho Yako Inakuja, anadaiwa kuwa ndiye kiunganishi cha uhusiano wa Lizy na Basila.
“Elizabeth na Basila walikutana kwa sababu ya Madam Ruth, yeye ndiye kama mshenga. Ndiyo maana wawili hao wakakaa na kuamua kufanya maandalizi ya kufunga ndoa,” kilisema chanzo.
Amani lilimsaka Madam Ruth kwa njia ya simu ili kutaka kujua ukweli wa madai hayo, alipopatikana alicheka na kumtaka mwandishi wetu kumuuliza habari za utumishi wake kwa Mungu badala ya uhusiano wa mtu na mtu.
“Niulize kuhusu kazi zangu za kumtumikia Mungu, si uhusiano wa mtu na mtu,” alisema.
Hivi karibuni, gazeti hili liliwahi kuripoti kwamba, Lizy na Basila walikuwa mbioni kufunga ndoa baada ya ile ya kwanza na Bahati kufeli safarini. Basila alikanusha, Elizabeth yeye alitaka kumjua aliyetoa habari hiyo Global bila kusema kweli au si kweli.

No comments:

Post a Comment