MWANAMITINDO kiwango Bongo, Hamisa Hassan Mobeto
amepangua tuhuma ambayo amekuwa akitupiwa na watu wanaomuona aking’aa
kisha kudai anatumia mgongo wa wanaume tofautitofauti (mabuzi).
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Hamisa alisema amekuwa
akisikitishwa na tabia hiyo ya watu kumnanga kwenye mitandao ya kijamii
kuwa anatupia picha nyingi ili kujiuza kwa mabuzi kitu ambacho si cha
kweli.
“Kiukweli asiyekujua hakuthamini, nasema hivi kutokana na watu wengi
wamekuwa wakinisema vibaya hasa katika mitandao ya kijamii, wanikome
kwani kila mtu ana maisha yake na mimi sitegemei mabuzi kuishi mjini,
nina mpenzi wangu mmoja tu,” alisema Mobeto.
No comments:
Post a Comment