Pages

Saturday, January 17, 2015

Hollande: Ufaransa itaendeleza vita dhidi ya magaidi

 Hollande: Ufaransa itaendeleza vita dhidi ya magaidi
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amesema leo kuwa, kumeanzishwa mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi na kusisitiza kwamba, operesheni ya kijeshi ya kimataifa dhidi ya makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka itashika kasi zaidi licha ya shambulio la hivi karibuni mjini Paris lililopelekea  kuuawa watu wasiopungua 17.
Rais Hollande ameyasema hayo mbele ya wanadiplomasia wa kigeni walioko mjini Paris na kudai kuwa, vita na mapambano hayo hayafanyiki dhidi ya dini, bali ni mapambano dhidi ya chuki na uadui. Rais wa Ufaransa amesema kuwa, majeshi ya nchi hiyo yanaendelea kuwasaka watu wanaoshirikiana na makundi ya kigaidi ya al Qaeda na Daesh ambayo yamejitangaza kuwa yana mfungamano na watu waliotekeleza mashambulizi ya Paris. Rais Hollande amesisitiza kwamba, kukaririwa vitisho vya kufanyika operesheni za kulipiza kisasi hakutazuia kutekelezwa operesheni hizo. Rais wa Ufaransa amezitaka nchi za Ulaya kuchukua hatua za pamoja za kukabiliana na makundi ya kigaidi.

No comments:

Post a Comment