Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul
‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa
faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo,
Aunty Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Iyobo ambaye
nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na
kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa
hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu
napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama
na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.
CHANZO: GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment