Na Erick Evarist/Ijumaa
MIEZI michache tangu ahamishie makazi yake nchini Afrika Kusini, modo
aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametia aibu kutokana na
kudaiwa ‘kujiuza’ kwa njia ya mtandao nchini humo.
Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza ubuyu kuwa,
Masogange yupoyupo tu, kazi kujipiga picha za utupu na kuzitupia
mtandaoni kana kwamba anatafuta wanaume.“Kimsingi hana kazi huku Sauz
zaidi ya kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram na anachanganya sana
wanaume wenye pesa zao, si unajua tena mtoto kajaliwa shepu la maana.
Baada ya chanzo hicho kuvujisha ubuyu huo, paparazi wetu aliingia
kwenye akaunti ya mrembo huyo na kujionea picha kibao zenye mapozi ya
kihasara. Jitihada za kumpata ili azungumzie madai hayo hazikuzaa
matunda kwani simu yake haikuwa hewani lakini katika maelezo yake kwenye
mitandao ya kijamii amewahi kudai anasoma chuo ingawa haijajulikana ni
chuo gani.
No comments:
Post a Comment