STAA wa filamu nchini, Wastara Juma amesema
anajihisi kupoteza mwelekeo unaomfanya kushuka kisanaa tokea kufariki
kwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kwani ari yake ya kufanya kazi
imepotea.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, alisema Sajuki alikuwa
ni msaada mkubwa sana kwake kisanaa mbali na maisha ya kawaida, kwani
anashindwa kupita njia alizokuwa anapitishwa na mumewe huyo kiasi cha
kujikuta akitoa filamu kati ya mbili hadi tatu kwa mwaka.
“Nikiri tu kwamba nimeshuka kisanaa, kasi ya kipindi kile imepungua,
mume wangu alikuwa akijituma kuhakikisha mikakati yetu inaenda, kwa
mwaka mzima nilitoa filamu hata tatu lakini toka asa naambulia moja tu
mwaka mzima,” alisema.
No comments:
Post a Comment