Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amekanusha taarifa zilizoandikwa
kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini likiwemo gazeti la Mtanzania
kuwa amempeleka Diamond polisi kwa kile kinachosemwa ni kumtapeli shilingi
milioni 10.
Martin ameiambia Mtandao wa Bongo5 kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote
na kwamba habari hizo ni za uongo.
“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani,” amesema Martin. “Kwa
sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts, kwahiyo sisi
tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori. “We don’t have any issue with Diamond.
Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.
“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa na nani ni
uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika zinaamua kuandika story
bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza ukweli wa hiyo story.”
BONYEZA HAPA KUSOMA ===>WEMA AMPELEKA DIAMOND POLISI, KISA NI DENI
No comments:
Post a Comment