MREMBO kunako tasnia ya filamu Bongo, Tamrina
Mohamed Poshi ‘Amanda’ ameshindwa kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa
mwanamuziki wa Bongo Fleva, Moses Bushagama aliyefariki mwishoni mwa
wiki iliyopita mkoani Dodoma kutokana na kuugua ghafla.
Akizungumza na Uwazi kwa masikitiko, Amanda ambaye pia ni mtu wa
karibu na marehemu, alisema kuwa alishapanga kusafiri kwenda Dodoma kwa
ajili ya maziko lakini kitendo cha kuugua ghafla kimeharibu kila kitu.
“Imeniuma sana kwa sababu ya ugonjwa wa taifodi kuniandama ambapo
nilikuwa nikitapika mfululizo,” alisema Amanda.Mez B alikuwa akiumwa
ugonjwa wa homa ya mapafu, alikuwa amelazwa katika Hospitali ya
Mwananchi kabla ya umauti kumkuta. Amezikwa Jumatatu katika makaburi ya
Wahanga mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment