Na Hamida Hassan/Ijumaa
Staa wa filamu za
Kibongo, Tiko Hassan amesema kuwa anatamani kupata mtoto wa pili kwa
sababu mtoto wake wa kwanza amefikisha miaka 10, tatizo hana wa kuzaa
naye.
Akipiga stori na Ijumaa Tiko alisema yeye ni ‘mgonjwa’ wa watoto
wachanga na anahisi sasa ni muda muafaka ila tatizo mwanaume aliyenaye
hana mpango wa kupata mtoto.
“Yaani acha tu, mpenzi niliyenaye naona kama hajajiandaa maana hata
nikiongelea ishu ya kubeba mimba, naona ananipotezea lakini kiukweli
nahitaji mtoto wa pili,” alisema Tiko.
No comments:
Post a Comment