Tasnia ya filamu Afrika inakuwa kila siku kiasi kwamba zile ndoto za
kufanya kama wenzetu wa Hollywood (Marekani) na Bollywood (India) huenda
siku moja zikatimia.
Kama ilivyo Hollywood na kwingine kwenye waigizaji wa kike wenye
mvuto, wapo pia waigizaji wa kike Afrika ambao ni ‘visu’.Leo hii
ikihitajika Top 10, kila mmoja atakuwa na yake lakini mtandao wa
umefanya kazi ya kuorodhesha waigizaji 10 wa kike wenye mvuto kama
ifuatavyo;
10. Elizabeth Michael ‘Lulu’
Binti huyu ana umri wa miaka 21 lakini ni mrembo na anayejiamini. Ni
binti kutoka Tanzania mwenye kipaji cha kuigiza kiasi cha kuwa tishio
kwa wakongwe. Ni kweli huwa anatumia ‘make up’ lakini hata akiwa
hajatumia wala kuvaa ‘mawig’, bado anaonekana ni mwenye kuvutia.
Ni mmoja wa mastaa wa kike nchini Nigeria mwenye mvuto wa aina yake.
Kwa sasa ana umri wa miaka 37 na watoto wanne lakini bado anaonekana
mrembo kiasi cha baadhi ya mashabiki wake kumuita Omosexy.Kutokana na
kipaji alicho nacho, amejikuta akiwa na mashabiki wengi katika Bara la
Africa na kwingineko duniani. Mbali na uigizaji pia ni mwanamitindo na
mwananamuziki.
Huyu ni muigizaji anayetokea nchini Ghana. Katika orodha ya waigizaji
wa kike waliomo nchini humo, mrembo huyu amebaki kuwa tishio na
imemfanya kuingia katika orodha hii ya wasanii wa kike wakali Afrika.
Huyu ni muigizaji kutoka Tanzania mwenye mvuto wa aina yake. Kwa
mujibu wa maelezo yake, uzuri alionao unatokana na mfumo mzuri wa kula
aliojiwekea. Anakula sana mbogamboga, matunda na maji mengi, hali
inayomfanya autunze urembo alionao.
Ana umri wa miaka 36, anatokea Nigeria. Mwanadada huyu anatajwa kuwa
na mvuto wa aina yake kiasi cha kupata usumbufu kutoka kwa wanaume
kibao.Ameigiza filamu nyingi na zote amezitendea haki kutokana na namna
anavyouvaa uhusika.
Amezaliwa miaka 32 nchini Canada lakini amekulia nchini Ghana. Ni
binti mrembo na mwenye kipaji ambaye aonekanapo kwenye televisheni,
huthibitisha kwamba kuna kitu cha ziada alichojaaliwa na Mungu.
Huyu ni msanii kutoka Ghana aliyezaliwa miaka 30 iliyopita. Licha ya
umri kusogea, hachuji kwa uzuri. Amecheza filamu nyingi na kadiri siku
zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kuwa tishio kwenye tasnia ya uigizaji.
Hivi unaanzaanzaje kumuacha mrembo huyu pale unapotaja medemu wakali
kwenye tasnia ya filamu Afrika? Naamini huwezi, labda uwe na chuki zako
binafsi.Ana umri wa miaka 31 na ana uzuri wa asili unaomfanya atumike
kwenye filamu nyingi za Nigeria.
Huyu ni binti kutoka Nigeria ambaye wengi wanamtaja kuwa muigizaji
mwenye mvuto kuliko wote Afrika. Ana miaka 33, aliwahi kushiriki
mashindano ya urembo nchini Nigeria na kuibuka mshindi. Kuanzia hapo
amekuwa gumzo kwa uzuri wake na amekuwa akitumika sana kwenye filamu
nyingi.
Wafuatiliaji wa filamu za Nigeria watakuwa wanamjua vizuri binti
huyu. Ana miaka 40 lakini bado anadai. Kila sehemu ya mwili wake ina
muonekana wa kiurembo.
Angalia midomo yake, angalia macho na ngozi yake. Hakika ni kati ya waigizaji wa kike Afrika wenye mvuto wa aina yake.









No comments:
Post a Comment