STAA wa filamu Bongo, Kajala Masanja kupitia kampuni
yake ya Kay Intertainment, ameamua kuungana na mastaa kibao Bongo
katika kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’
yaliokithiri hivi sasa.
Akichezesha taya na Uwazi, Kajala na timu yake nzima wameunda kitu
kinachoitwa ‘Simama Nami’ ambapo tayari wameshatunga wimbo wa pamoja
walioshirikiana na Mwasiti, Shilole, Linah, Keisha, Zamaradi, Kadjanito
na wengine wengi.
“Kwa kweli mauaji hayo yananiumiza kila kukicha, nilifikiria
tutafanya nini hivyo nikaona bora tufanye hii kampeni ambayo naamini
mimi na wenzangu tutafanikiwa. Kampeni hii si ya leo tu bali ni
endelevu,” alisema Kajala.
No comments:
Post a Comment