Pages

Wednesday, March 4, 2015

Kenya yachoma kwa moto tani 15 za pembe za ndovu

 Kenya yachoma kwa moto tani 15 za pembe za ndovu
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya leo ameongoza Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani na Siku ya Wangari Maathai kwa kuteketeza kwa moto tani 15 ya pembe za ndovu zilizokuwa zikisafirishwa kimagendo. Sherehe hiyo iliyofanyika katika Mbuga ya Wanyama ya Nairobi ilihudhuriwa na wageni 1,000 akiwemo 
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, mawaziri, maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa na wawakilishi wa nchi mbali mbali duniani.


 Aidha leo pia ni Siku ya Mazingira Afrika ambayo huadhimishwa ili kufahamisha umma umuhimu wa kulinda mazingira ya bara Afrika. Kuanzia mwaka 2012 siku hiyo huadhimishwa pamoja na Siku ya Wangari Maathai ili kumuenzi mlinda mazingira hiyo wa Kenya aliyepata Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na jitihada zake za kulinda mazingira. 

Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa siku hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema biashara haramu ya wanyamapori na bidhaa zitokanazo na viumbe hivyo ikiwemo ndovu, magogo na kifaru, imekuwa ikiibuka na mbinu mpya kila uchao na hata kuzidi ile ya usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya.
 Amesema kushamiri huko kunapigiwa chepuo na rushwa na uongozi dhaifu akiongeza kuwa kuna ushahidi thabiti wa kuhusika kwa mitandao ya kihalifu iliyopangwa na vikundi vilivyojihami.

No comments:

Post a Comment