BAADA ya kuficha kwa muda mrefu huku akikanusha
kujifungua, hatimaye staa wa muziki wa mduara na sinema za Kibongo,
Snura Mushi ‘mama wa Hawashi’ ameamua kumwanika ‘live’ mwanaye
aliyejifungua hivi karibuni na kutoa sababu kuu ya kufanya hivyo.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, nyumbani kwake Mwananyamala, Dar,
Snura alisema kuwa yupo tayari kuonekana mbaya kusemwa lakini sababu
kubwa ya kumficha mtoto wake ilikuwa ni kazi yake ya muziki ambayo
anaitegemea kama baba wa familia yake.
“Ikumbukwe kuwa mimi ndiye baba na ndiye mama wa watoto pamoja na
familia yangu hivyo nililazimika kuficha kwa nia ya kuwaweka mapromota
wangu ambao kama ningetangaza nina mimba wasingenipa kazi kabisa na
huwezi kuamini nilikata nyonga mpaka nikiwa na miezi mitano ya
ujauzito,” alisema Snura.
Snura alitiririka kuwa kwa kawaida, kwa Tanzania, mwanamke akiwa na
ujauzito hasa muimbaji, kumpa kazi huwa ni vigumu hivyo alilifikiria
hilo kwa upana akaona hawezi kupata kazi haraka kwani kila atakayemtaka
ataambiwa ana mimba au amejifungua.“Kwa sasa nimeshakuwa fiti ‘so’
nimeamua kuweka wazi kwani nina uwezo wa kufanya kazi wakati wowote
nikiitwa,” alifunguka Snura.
AKUBALIANA NA MENEJA WAKE
Alisema: “Baada ya kuona siwezi tena
kupanda jukwaani, nilikaa na kumpa wazo meneja wangu (HK), tukapanga
nikiuliziwa aseme nimeenda Afrika Kusini kufanya video yangu lakini
ukweli nilijifungia chumbani nyumbani kwangu, chumba kilipewa jina la
kwa Madiba.
AJIFUNGULIA PALESTINA
“Nilijifungua katika Hospitali ya
Palestina iliyopo Sinza, Dar. Ilikuwa Januari 2, 2015. Niliingia
nimevaa nikabu na niliwatonya manesi kuwa nahitaji chumba cha peke
yangu. Kweli walinikubalia, nawashukuru sana kwa hilo, nilipata mtoto wa
kiume anayeitwa Taltham.”
MASTAA WALIOMFICHIA SIRI
Snura aliwataja mastaa waliomfichia
siri na kuwashukuru kuwa ni Halima Yahya ‘Davina’ aliyefanyia arobaini
nyumbani kwake, Tundaman, Amisuu Malick na wengine wachache.
Mwisho Snura aliwaomba Wabongo wamsamehe kwa kuwa alifanya hivyo kwa
sababu ya kazi na amewaomba mapromota wamtafute kwani kwa sasa amekuja
upya na mambo mapya huku akiwataka mashabiki watembelee ukurasa wa mtoto
wake wa Instagram kwa jina la Tsnura kwa ajili ya kujionea picha
zinazomuonesha kuanzia mimba mpaka mtoto alivyozaliwa.
No comments:
Post a Comment