DOKTA amempiga stop staa wa filamu Bongo, Aunt
Ezekiel kwenda kujifungulia nchini Marekani kwa sababu hali yake ya
ujauzito aliyofikia haruhusiwi kusafiri kwa kutumia usafiri wa anga
kwenda popote.
Chanzo makini kilisema kuwa, Aunt alijiwekea mpango wa kwenda
kujifungulia nchini huko kwa muda mrefu lakini alikuwa akisubiri mimba
ikue kidogo kitendo ambacho hakikutakiwa kwa kuwa ujauzito umekuwa
mkubwa na kusafiri kungemletea tatizo la presha ya kushuka.
“Imebidi nikubaliane na daktari alivyosema kwa kuwa wao wanajua
hivyo siwezi kupingana nao naogopa nisije kupata matatizo, bora
nijifungulie hapahapa nyumbani na nimelikubali hilo na mawazo ya nyuma
nimefuta japokuwa nilikuwa nimeandaa kila kitu kwa safari hiyo,” alisema
Aunt alipopigiwa simu.
Awali Aunt alipanga kwenda kujifungulia nchini Afrika Kusini lakini
baadaye aliahirisha baada ya kupata shavu kwa marafiki zake waishio
nchini Marekani waliomtaka kwenda kujifungulia huko na kukaa kwa miezi
mitatu.
No comments:
Post a Comment