Pages

Wednesday, April 22, 2015

HIVI WASANII MTAKUWA NA UCHUMBA‭, ‬NDOA ZA MAIGIZO MPAKA LINI‭?‬


Kwenu mastaa wa tasnia mbalimbali Bongo‭, ‬habari zenu bwana‭. ‬Poleni na majukumu ya kila siku ya kulijenga taifa‭.‬
Mkitaka kujua afya yangu‭, ‬mimi ni mzima‭, ‬namshukuru Mungu naendelea kutimiza majukumu yangu‭, ‬likiwemo hili la kuwaandikia barua‭.‬
Nimewakumbuka leo kupitia barua‭, ‬nataka kuwaambia kwamba mimi pamoja na mashabiki wengine wa sanaa yenu tumewachoka‭. ‬Tumechoka kuona na kusikia kila siku mkifanya maigizo kwenye maisha yenu halisi‭.‬
Hivi ni kwa nini kila kukicha tunasikia mnaachana‭? ‬Kwa nini hamdumu kwenye uhusiano wa mapenzi‭? ‬Kwa nini hamdumu kwenye ndoa kama mashabiki wenu wanavyowategemea‭?‬
Penzi linapoanza kushamiri‭, ‬mnalinadi kwenye mitandao na vyombo vya habari‭. ‬Mnawaaminisha mashabiki wenu kuwa mnapendana kwa kauli zenu motomoto lakini ndani ya miezi miwili mitatu penzi chali‭.‬Wengine mnaonesha kwamba mmedhamiria na kuamua kufunga ndoa kabisa‭, ‬lakini kumbe moyoni bado mnakuwa mna lenu jambo‭. ‬Mashabiki wenu wanafurahia kuona mmeoana lakini ndoa nayo haidumu‭, ‬mnaachana‭.‬
Mbaya zaidi mnapoachana mnapeana maneno ya kashfa‭, ‬mnaumbuana kiasi ambacho kinadhihirisha kabisa mlikuwa hamna mapenzi ya dhati‭ ‬au hamkudhamiria kabisa kuingia kwenye ndoa‭.‬Hivi kama kweli mlipendana‭, ‬nini kinawafanya muanze kuumbuana‭? ‬Badilikeni‭, ‬mashabiki wenu wamechoka kusikia kila kukicha ndoa ya‭ ‬staa fulani imevunjika‭, ‬wachumba fulani wameachana‭, ‬ni aibu‭.‬
Watu hawapendi kuona Nay wa Mitego na Siwema mkiwa mmeachana‭. ‬Tena mnaachana kwa kupeana maneno yanayoonesha kwamba mlikuwa hamna nia ya dhati ya kuwa wapenzi‭.‬Shamsa Ford na Dick‭, ‬kapo yenu ilikuwa nzuri‭. ‬Mlipamba vyombo vya habari‭, ‬uhusiano wenu ukazaa matunda ya mtoto mmoja lakini ndoto ya kuishi kama mume na mke imeyeyuka‭.‬
Nasibu Abdul‭ ‬‮!‬٪Diamond‮!&‬‭ ‬na Wema Sepetu penzi lenu lilikuwa likipendwa‭  ‬na wengi‭, ‬likaishia njiani‭. ‬Rose Ndauka na Malick Bandawe mlioishi na kubahatika kupata mtoto mmoja‭, ‬nini kiliwakuta‭? ‬Inasikitisha‭.‬Wolper na Dallas nao walipamba sana vyombo vya habari lakini mwisho wa siku chali‭. ‬Ndugu zangu‭, ‬mnapaswa kubadilika‭. ‬Msiigize maisha yenu‭. ‬Igizeni kwenye filamu‭, ‬mkirudi nyumbani mjitambue kwamba heshima‭, ‬upendo‭, ‬busara vinahitajika ili kuishi na mwenzako‭.‬
Mbona wapo wasanii wengi tu maarufu duniani na wamedumu kwenye uhusiano‭? ‬Kwa nini msiige mfano kwa mastaa kama Marlaw na mkewe‭, ‬Jay Z na Beyonce ambao wanaheshimu penzi lao hadi sasa‭?‬Jamani‭, ‬cha msingi mnapaswa kuheshimu suala la uhusiano‭, ‬msifanye masihara katika maisha ya ukweli‭.  ‬Vitu vingine vinapaswa kufanyika kwenye filamu pekee na siyo kuvihamishia katika maisha halisi‭.‬
Bila shaka mtakuwa mmenielewa na mtabadilika‭, ‬kila la kheri‭.‬

No comments:

Post a Comment