STAA mkongwe wa sinema za Kibongo, Ruth Suka
‘Mainda’ ametoa ushuhuda mzito (confession) baada ya kukiri kuishi
maisha ya starehe ikiwemo unywaji pombe na kukosea mwanaume sahihi wa
maisha kwa kuingia kwenye uhusiano tofauti jambo aliloliita ni
‘kumtumikia shetani kwa pombe na ngono’.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu hivi karibuni katika
mahojiano maalum, Mainda ambaye kwa sasa ni mlokole wa ‘tuimbe na
kusifu’ aliweka wazi kuwa kipindi cha nyuma, shetani alimzidi nguvu kwa
kujichanganya maeneo ya baa na kunywa pombe jambo ambalo kwa sasa kila
akikumbuka huishia kusikitika.
Alisema, kwa sasa hana mpenzi na kwamba hatafuti lakini anamngojea
yule ambaye anaamini atatoka kwa Mungu kwa wakati muafaka.Mainda aliweka
wazi kuwa anamshukuru Mungu kwa kumuongoza katika njia nyoofu huku
akiainisha kuwa maisha bila ya kuwa na Mungu ni ya ajabu sana.
“Kwa kweli maisha ya zamani yalikuwa ya ajabu, ulevi wa pombe, kutoka
na wanaume tofauti nikidhani ndiye mwanaume sahihi, zilikuwa ni nguvu
za shetani, namshukuru Mungu kwa kunibadilisha kwa kiwango hiki kwani
nilimtumikia sana ibilisi kwa mambo machafu, viongozi wangu wa dini
wananipa mwanga mkubwa mno juu ya Neno la Mungu na kila nikikumbuka
maisha ya nyuma, huwa siyatamani kabisa,” alisema Mainda.
No comments:
Post a Comment