Pages

Wednesday, June 24, 2015

MTITU AKUBALI KUSAMEHEANA NA STEVE


MTITU42 
Staa wa filamu Bongo, William Mtitu.
Brighton Masalu
KUJISHUSHA! Staa wa filamu Bongo, William Mtitu amesema yupo tayari kumaliza ugomvi na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kutokana na shinikizo kutoka kwa wasanii wenzake, wadau na mkewe.
Kwa mujibu wa chanzo makini, kikao kizito kikimhusisha Mtitu na wasanii nguli kiliitishwa na kumuonya juu ya suala hilo kabla ya kukubali kuwa yuko tayari kumalizana na Steve.
steve 
Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Kilikuwa ni kikao kizito kaka, Mtitu ‘alipewa vipande’ vyake huku wasanii wakimpa hasara za mabifu yasiyokuwa na faida na yeye alielewa, na sasa yuko tayari kwa suluhu,” alisema mmoja wa wasanii mwenye jina kubwa.
Mwandishi wetu alimtafuta Mtitu ili kusikia chochote kutoka kwake ambapo alisema;
“Duh! Umeipata na hiyo! Ni kweli kabisa, hakuna haja ya kuwa na mabifu katika zama hizi za maisha mafupi, wakiandaa mpango wa kutukutanisha, niko tayari.”
Kwa upande wake, Steve Nyerere alisema asingeweza kulizungumzia suala hilo kwa wakati huo kwani alikuwa na kazi anaifanya. Aliahidi kumtafuta mwandishi baadaye, lakini hadi Risasi Mchanganyiko linakwenda mitamboni, alikuwa hajawasiliana naye.

No comments:

Post a Comment