NYOTA mkubwa katika Bongo Movies,Vincet Kigosi ‘Ray’
ameweka wazi kuwa Chuchu Hans, ambaye ni mpenzi wake wa muda mrefu, si
mpita njia, bali ni mwanamke anayesubiri ndoa kwa kuwa ana sifa zote za
kuwa mke.
Kwa sababu hiyo, alisema siyo jambo zuri kufikiri kila anapotoka
katika mitoko yake ya usiku awe naye kwa kuwa mke hafai kuwa mtu wa
kuzunguka naye usiku kama hakuna ulazima wa kufanya naye hivyo.
“Kama hivi, mimi nimekuja hapa kwenye shughuli ya ZIFF, kitu hiki
kinanihusu peke yangu, hakuna haja ya kumsumbua kuja naye, yule ni mke,
siwezi kumtembeza pasipo ulazima wa kutufanya kuwa pamoja,” alisema.
No comments:
Post a Comment