Brighton Masalu
MTANGAZAJI wa
ITV / Radio One, Farhia Middle amesema tangu aujue ulimwengu wa mapenzi
hajawahi kukutana na mwanaume mwaminifu na kwamba kila mara amekuwa
akilizwa na mapenzi jambo ambalo husababisha kujiona mwenye mkosi.
Akipiga stori na gazeti hili hivi karibuni, mtangazaji huyo alisema
licha ya baadhi ya watu kumsifia kuwa ni mrembo kwa sura na umbo, lakini
amekuwa akikutana na balaa la kuumizwa na mapenzi kwa kusalitiwa ama
kunyanyaswa na wanaume.
“Yaani huwezi amini, wakati mwingine huwa najiuliza kwa nini mimi?
Mbona kila mwanaume ninayempata sidumu naye. Kama siyo msaliti basi ni
yule mwenye mfumo dume na hulka za kunyanyasa. Najiona kama nina mkosi,”
alisema Farhia.
No comments:
Post a Comment