Pages

Tuesday, August 28, 2012

WAZIRI NCHIMBI, DK. REGINALD MENGI WAONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA MZEE BUKUMBI DAR




Mwili wa marehemu Mzee James Bukumbi ukishushwa kwenye gari nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar jana.
Waombolezaji wakiwa na simanzi wakati mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake.
Mjukuu wa marehemu, Samwel Shigongo akiwa amebeba msalaba.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akimpa pole Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric James Shigongo aliyefiwa na baba yake. Katikati ni Meneja wa Global, Abdallah Mrisho. Nape akisaini katika kitabu cha rambirambi.
Nape akisalimiana na msanii Mrisho Mpoto.
Kiongozi wa Bendi ya Extra Bongo, Alli Choki (kushoto) akisalimiana na Eric Shigongo.
 
Jeneza lenye mwili wa Marehemu, Mzee James Bukumbi.
Ibada ya kumuombea marehemu ikiendelea.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akibadilishana mawazo na Eric Shigongo wakati wa chakula.
Mamia ya wakazi wa jiji la Dar, jana walikusanyika nyumbani kwa marehemu, Mzee James Bukumbi ambaye ni baba mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric James Shigongo kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho. Marehemu aliyefariki dunia  usiku wa kuamkia Jumapili Agosti 26, 2012, aliagwa nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam na leo amesafirishwa kuelekea jijini Mwanza kwa mazishi.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments:

Post a Comment