Pages

Friday, November 30, 2012

CHAMA cha Washereheshaji Nchini (Sherehe Arts Association –SAA) yatoa rambi rambi kwa Sharomilionea

CHAMA cha Washereheshaji Nchini (Sherehe Arts Association –SAA), kinatoa pole za rambirambi kwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, familia ya Marehemu Hussein Ramadhan 

‘Sharomilionea’ kutokana na kifo cha msanii huyo.
Rambirambi hizo zimetolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, MC Bryceson Makena, alipokuwa akizungumza na mwanadishi wa habari hizi.

Alisema SAA inawatakia wanafamilia wote ujasiri wa kulipokea jambo hilo na kuvuta subira kwani wote njia ni moja ila wakati ndio tofauti.Pia ametoa wito kwa wasanii wote nchini kuwa na umoja na mshikamano endelevu katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

Post a Comment