Pages

Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA.

Habari ambazo zimetufikia hivi punde zinapasha kwamba muigizaji na mwanamuziki, Hussein Ramadhan Mkieti almaarufu kama Sharo Milionea,amefariki dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea mida ya saa mbili usiku wa kuamkia leo katika eneo la Maguzoni Songa katikati ya Segera na Muheza mkoani Tanga.
Habari za ajali hii na tukio hili la kusikitisha zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe. Kwa mujibu wa Kamanda huyo, gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BBR alilokuwa akiendesha marehemu kutokea Dar-es-salaaam kwenda Muheza lilipofika katika eneo hilo liliacha barabara na kupinduka na hivyo kusababisha mauti yake.Mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali Teule ya Muheza.
IRENE MWAMFUPE JAMII inaungana na wapenzi wote wa sanaa nchini Tanzania kutoa pole za dhati kwa ndugu,jamaa na marafiki wa Sharo Milionea.Pumzika kwa Aman

No comments:

Post a Comment