Pages

Tuesday, November 27, 2012

WASANII WA KOMEDI WAMLILIA SHARO MILIONEA.

WASANII wa filamu za vichekesho hapa nchini, jana walionyesha kusikitishwa kwao na kifo cha msanii mwenzao, Sharo Milionea kilichotokea Muheza, Tanga kwa ajali ya gari jana usiku.
Wakizungumza na saluti5 Mwananyamala kwenye msiba wa John Maganga, wasanii Kitale, Bingwa Rivaz, Maringo Saba, Mkono, Eric na wengine wengi, walisema wamepoteza jembe katika fani yao.
“Wasanii wengi wa komedi haswa sisi vijana bado ni masikini sana na hatuthaminiwi, lakini Sharo tayari alikuwa ni balozi wetu katika njia kutukomboa kutoka hali ya kudharauliwa hadi hadhi za juu” alisema Maringo Saba wa kipindi cha Mizengwe cha ITV.
“Sharo alionyesha njia, alitufungua macho kuwa komedi ukiipeleka kwenye muziki ina lipa na sote tulikuwa nyuma yake, alikuwa anatupa changamoto na kila mtu alitamani kuwa yeye” anasema Alex wa Machejo “Bingwa wa Rivaz”.
Erick anaye igiza sauti ya kitoto kwenye komedi zinazorushwa Channel 10 nayependa alisema Sharo ni tochi itakayoendelea kuwamulikia njia kwa miaka mingi ijayo”.
Kwa ujmla kila msanii alijaribu kuonyesha kuwa Sharo alikuwa mtu wa watu na jinsi ambavyo pengo lake haliwezi kuzibika.Via saluti5.com

No comments:

Post a Comment