Pages

Thursday, November 29, 2012

WOLPER: NIKIACHIKA TENA, NATIMKA BONGO NA KWENDA UGHAIBUNI KUOLEWA HUKO.

PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa ughaibuni.Akiteta na Tollywood Newz hivi karibuni jijini Dar, Wolper alisema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka  tena kuwa na mpenzi wa  Kibongo.
 
“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi.Ikitokea sitakuwa na amani moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas’.Chazo cha hii habari ni Gazeti pendwa la Risasi Mchanyiko uk wa 3.

No comments:

Post a Comment