Pages

Saturday, December 1, 2012

‘TUTARUDISHA KODI YA PANGO YA SHARO MILIONEA’.

CHANZO CHA HABARI HII NA SALUTI5 (www.saluti5.com)
WAMILIKI wa nyumba aliyokuwa akiishi msanii wa Komedi, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ wamesema watarudisha kiasi chote cha fedha ya kodi ya pango kilichotolewa na nyota huyo.
Wakiongea na Saluti5 jana, wamiliki hao wameahidi kukabidhi pesa zote za kodi ya pango zilizokuwa zimelipwa na Sharo, siku vitakapokuwa vinatolewa vyombo.

“Hatuwezi kuzuia hela iliyotolewa na Sharo kama kodi ya pango kwa sababu kitendo hicho ni sawa na dhuluma ambayo ni kosa kwa mujibu wa dini yetu ya Kikristo,” walisema wamiliki hao.


Walisema kuwa, watairudisha kodi hiyo kwasababu Sharo alihamia kwenye nyumba yao takriban wiki moja tu kabla ya ajali iliyosababisha mauti kumfika.
Nyumba aliyoishi Sharo kwa wiki moja tu maeneo ya Sinza B, Dar es Salaam
Sehemu nyumba aliyokuwa akiishi Sharo, Sinza B, geti jeusi ndio la kuingilia kwenda kwenye nyumba ya ndani aliyopanga msanii huyo.
Hii ndio nyumba ya kina Sharo Milionea ya kule Lusanga, Muheza
Jirani zake na Sharo hapo Sinza B ambao nao walifiwa siku hiyo hiyo aliyofariki msanii huyo
Nyumba nyingine tena jirani na Sharo ambao na pia walifiwa siku hiyo hiyo
Mnoko: Fundi Cherahani, mpangaji mwenzake na Sharo akijificha asipigwe picha, fundi huyu alijitahidi kuzuia bila mafanikio mahojiano ya Saluti5 na mama mwenye nyumba. 
                CHANZO CHA HABARI HII NA SALUTI5 (www.saluti5.com)

No comments:

Post a Comment