Pages

Saturday, January 26, 2013

BEN POL, LINAH KUPIGA BONGE LA SHOW VALENTINE DAY …KIINGILIO LAKI MOJA


KAMPUNI ya Keys Production, imeandaa onyesho kabambe ndani ya Jangwani Sea Breeze, litakalopambwa na wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ben Pol na Linah.
Mmoja wa wasemaji wa kampuni hiyo ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo maalum kwa wapendano litafanyika Alhamisi ya terehe 14 mwezi ujao, siku ya Wapendao Duniani (Valentine day) ambapo kwa wale watakaojisikia kukaa sehemu ya VIP, watalazimika kulipa kiingilio cha sh. 100,000 za kibongo.
Kiingilio cha kawaida katika onyesho hilo litakalopambwa pia na Live Band kitakuwa ni sh. 20,000.
Onyesho hilo litakaloanza saa 1 za usiku linatarajiwa kuwa la aina yake, likipambwa na nyimbo za mahaba huku watu wakipata fursa ya kucheza na maji katika bwawa la kuogelea.
                                             CHANZO SALUTI 5

No comments:

Post a Comment