Pages

Saturday, January 26, 2013

Bonanza la Polisi Moro leo

JESHI la Polisi mkoani Morogoro, linatarajiwa kufanya bonanza kwa ajili ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribishwa 2013 kwenye Bwalo la Umwema lililoko mjini hapa, leo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Kituo cha Polisi mkoani 

Morogoro (OCS), Idd Ibrahim, alisema kuwa bonanza hilo linatarajiwa kushirikisha familia za jeshi hilo na wadau mbalimbali, ikiwemo waandishi wa habari.
“Katika bonanza hili la kuukaribisha mwaka 2013, kutatanguliwa na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kati ya jeshi hilo na waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro,” alisema Ibrahim.

Aidha alisema kuwa, michezo mingine ni pamoja na netiboli kati ya askari wa kike na wake za askari, kukimbiza kuku na mingineyo, ambapo imepangwa kufanyika asubuhi kwenye uwanja wa Jamhuri.
“Michezo hiyo tunatarajia kuifanya asubuhi huku ikiongozwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile,” aliongeza.
Hata hivyo, mara baada ya kukamilika kwa michezo hiyo, kutafuatiwa na tafrija fupi itakayofanyika Bwalo la Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Umwema, mjini hapa.

No comments:

Post a Comment