Pages

Thursday, January 3, 2013

CHELSEA YACHAPWA NA VIBONDE ...YAMSAJILI DEMBA BA, LIVERPOOL YAUA 3-0

CHELSEA jana usiku iliweka rehani juhudi zake za kusaka ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuchapwa 1-0 na timu iliyopo mkiani, QPR.
Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Shaun Wright Phillips, ndiye aliyekuwa mwiba kwao kufuatia bao lake la dakika ya 78 lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo uliofanyika katika dimba Stanford Bridge.

WRIGHT STUFF ... Hoops hail hero SWP
Shaun Wright Phillips baada ya kuitungua Chelsea
Kwa goli hilo la Phillips aliyesaliwa na Chelsea mwaka 2005 kwa ada ya pauni milioni 21 kutokea Manchester City, Kocha wa QPR Harry Redknapp sasa anaamini amepata fomula ya kuinusuru timu yake na janga la kushuka daraja.


“Ushindi dhidi ya Chelsea ni ushindi bora zaidi katika maisha yangu ya soka” alisema Redknapp ambaye timu yake ilipaki bus langoni mwake kwa muda wote wa mchezo.
Mabao mawili ya Luis Suarez na moja la v Raheem Sterling yalitosha kuipa ushindi mnono Liverpool wa bao 3-0 dhidi ya Sunderland huku Newcatsle ikipokea kipigo cha 2-1 kutoka kwa Everton.

Luis Suarez and Matthew Kilgallon
Luiz Suarez akichanja mbuga
Daniel Sturridge
wa Liverpool Daniel Sturridge akiufuatilia mchezo
Raheem Sterling
Raheem Sterling akiifungia Liverpool bao la kwanza
Wakati huo huo, Chelsea jana ilikamilisha usali wa mshambuliaji wa Newcastle, Demba Ba kwa uhamisho wa ada ya pauni milioni 7.5 na mshahara wa pauni 75,ooo kwa wiki.
Demba Ba, kifaa kipya cha Chelsea

No comments:

Post a Comment