Pages

Thursday, January 3, 2013

KIFO CHA SAJUKI: INATAKA MOYO KUMKABILI WASTARA

HALI ya mke wa Marehemu Sajuki, Wastara Juma ni ya kusikitisha na inahitaji moyo mgumu kukaa nae na kumfariji.
Wastara alipitisha siku nzima ya jana akilia bila kupumzika, karibu kila msanii aliyeingia chumbani mwake kwenda kumsalimia alikutana na kilio cha Wastara.
Mh. January Makamba akijaribu kumfariji Wastara

Mkurugenzi wa Clouds, Ruge Mutahaba nae akimfariji Wastara
Hali hiyo ilipelekea baadhi ya wasanii kuhofia kwenda kumsalimia kwa kuamini kuwa watakuwa wanaenda kumliza upya badala ya kumfariji.
Saluti5 ilipojaribu kuingia chumbani kwa Wastara ikiwa imeongozana na wasanii Mrisho Mpoto, Issa Mussa “Cloud” na Lumole Matovolwa “Big” ilikutana na kilio kizito na hakuna aliyethubutu kupoteza hata dakika mbili chumbani humo.
Jaqline Wolper, mmoja kati ya watu waliotoa mchango mkubwa wakati wa kumuuguza Sajuki
Mohamed Said, mdogo wa marehemu, ambaye ndiye aliyekuwa akimuuguza Sajuki hospitalini hadi kifo chake
Historia ya wasanii hao wawili (Sajuki na Wastara) iliyopitia misukosuko na mitihani mikubwa, inafichua penzi zito na la kweli miongoni mwao, hali ambayo itamfanya Wastara asikaukwe na chozi kwa muda mrefu wa maisha yake.
Zamaradi Mketema wa Clouds TV (mwenye begi katikati) akiwa na waombolezaji wengine jana nyumbani kwa marehemu Sajuki
Umati uliofurika kumboleza msiba wa Sajuki
Sajuki alifariki jana alfajiri kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na anatarajiwa kuzikwa kesho mchana kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment