Pages

Thursday, January 3, 2013

WEMA BADO AWEWESEKEA PENZI LA KANUMBA

Na Imelda Mtema
MSANII wa filamu Bongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ameonekana kuliwewesekea penzi la aliyewahi kuwa laaziz wake, marehemu Steven Kanumba baada ya kufunguka kuwa hatatokea mwanaume kama yeye.
Wema Sepetu.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wema alisema amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume kadhaa lakini penzi ambalo lilikuwa na hisia kali ni lile la kwake na Kanumba tu.
Mrembo huyo aliongeza kuwa yeye na marehemu walikuwa na matarajio mengi na anaamini angekuwa hai lazima wangekuja kuoana kwani walikuwa wakipendana kwa dhati.
Wema Sepetu akiwa na mpenzi wake wa zamani, marehemu Steven Kanumba.
“Yaani kusema ukweli hakuna ‘kapo’ nitakayoipata ifanane na ya Kanumba mpaka naingia kaburini, tena kama angekuwa hai lazima tungekuja kuoana, tulikuwa tukipendana ajabu,” alisema Wema.
                                   CHANZO CHA HABARI NI GLOBAL PUBLISHERS.

No comments:

Post a Comment