Pages

Wednesday, January 2, 2013

MATOKEO MECHI ZA JANA UK

WIGAN 0 MAN UNITED 4
Javier Hernandez Chicharito na Robin van Persie leo wakiwa ugenini wameifunga timu ya Wigan goli 4 kwa 0, Goli hizo 4 zimefungwa kipindi cha kwanza na cha pili. Kila mmoja akifunga goli 2 na kuwapa Vinara wa Ligi Manchester United ushindi wa Bao 4-0 walipocheza ugenini na Wigan na kuwabakiza kileleni wakiwa Pointi 7 mbele ya Man City.

Chicharito akipongezwa baada ya kufunga goli
Hernandez akifunga goli kipindi cha kwanza dakika ya 35
Hadi mapumziko Man United walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao la kwanza la Chicharito baada ya shuti la Patrice Evra kutemwa na Kipa wa Ali Al Habsi na kutua kwa Chicharito aliemalizia vizuri.
Robin van Persie alifunga Bao la pili tamu sana baada ya kumgeuza nje ndani Beki wa wa Wigan Ivan Ramis na kupinda shuti lake lililomshinda Kipa.
Kipindi cha Pili Chicharito alifunga Bao la 3 kufuatia frikiki ya Van Persie kuwababatiza Mabeki wa Wigan na Bao la 4 kufungwa na Van Persie alipopokea krosi safi ya Danny Welbeck.

Robin van Persie akitupia nyavuni.

Robin Van Persie akiangalia mpira ukitumbukia golini.

Rvp akishangilia.
Sir Alex Ferguson akifurahia ushindi huo DW Stadium leo hii.

VIKOSI:
WIGAN: Al Habsi, Ramis, Caldwell (Stam 69), Figueroa, Boyce, McCarthy, McArthur, Beausejour, Di Santo (Gomez 70), Maloney (McManaman 86), Kone.
Subs Not Used: Pollitt, Jones, Boselli, Golobart.
Booked: Caldwell.
MAN UNITED: De Gea, Da Silva, Ferdinand (Smalling 68), Evans, Evra, Young (Welbeck 78), Carrick (Kagawa 68), Cleverley, Giggs, Van Persie, Hernandez.  
Subs Not Used: Lindegaard, Valencia, Vidic, Scholes.
Booked: Smalling.
Goals: Hernandez 35, 63, Van Persie 43, 88
Attendance: 20,342
Referee: Andre Marriner


MATOKEO MECHI ZA LEO
Jumanne 1 Januari 2013
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom 1 v Fulham 2
[SAA 12 Jioni]
Man City 3 v Stoke 0
Swansea 2 v Aston Villa 2
Tottenham 3 v Reading 1
West Ham 2 v Norwich 1
Wigan 0 v Man United 4
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton 1 v Arsenal 1


RATIBA LEO:
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

No comments:

Post a Comment